Page 8 - seven (1)
P. 8
3. Pesa za kuanzisha biashara huitwa____.
4. Karo ni kwa shule kama vile nauli ni kwa ____. (usafiri, gari, shambani)
5. Kila baada ya mwezi, mwalimu wetu hupokea ____mkubwa.
Mapambo
Je, mapambo haya huvaliwa wapi?
1. Furungu
2. Kikuku
3. Kibanio
4. Mshipi
5. Mapete
6. Kishaufu
7. Kidani
Nomino za jamii
Pia huitwa nomino za makundi.
Mifano:
1. Thurea ya nyota
2. Chane ya ndizi
3. Tone la maji.
4. Shada la maua.
Zoezi:
1. Katika sherehe ya mahafali, kila mtu alikuwa na ___ la maua shingoni.
2. Mchajakuni ameuza tita la __ kwa bei ya juu mno.
3. Mwanafunzi anatakiwa kuyabukua ___ya vitabu,
4. Naomba walau ___la maji. Kiu inaniangamiza.
5. Shungi ni kwa nywele kama vile kishazi ni kwa ____
6. Kamilisha: Genge la vibarua au_______
JUMA LA TATU
KIPINDI CHA KWANZA: KUANDIKA
KUANDIKA:
INSHA YA MASIMULIZI
Idara ya Kiswahili Tender Care Junior Academy

